Mimi ni wewe. Wewe ni mimi.
Kama wewe ni kijana, afisa ugani au mjasiriamali mwenye ujuzi wa kilimo, huu ni wakati wako. MazaoHub tunatoa nafasi ya kipekee kupitia mfumo wetu wa Tech & Touch, ili kukujengea msingi endelevu wa kuhudumia wakulima kwa kutumia data halisi, masoko halisi, na kipato halisi.
Huko mkoani Manyara, tayari wakulima wamechagua Tech & Touch kwa sababu wanaona thamani yake, kuanzia maandalizi ya shamba hadi mavuno, pamoja na wanunuzi wa mazao wakiwa tayari baada ya mavuno.
Wakulima wanalipia kwa sababu wanaona matokeo. Na sasa tunaeneza mfumo huu uliothibitika nchi nzima kupitia wewe kwa njia ya mafunzo na kwa lengo la kupatia kipato wewe kijana wa kitanzania.
Manufaa ya kuwa Partner na mtoaji wa huduma za Ugani wa MazaoHub
Utapatiwa mfumo wa MazaoHub (Pro license): Ambapo kuna aina nyingi za mazao, akili bandia ya uchambuzi wa udongo, rekodi za shamba, mipango ya mazao iliyoandaliwa, na vifaa vinavyofanya kazi hata bila mtandao(offline) ndani ya app ya MazaoHub.
Utapata orodha ya agrovets washirika waliohakikiwa. Ukiwezeshwa kusambaza au kununua pembejeo za kilimo kwa ajili ya wakulima wako, huku unapata kamisheni.
Utaweza kuhifadhi data za wakulima: Hudumia wakulima waliothibitishwa katika eneo lako toa majibu ya vipimo vya udongo, mipango ya mazao, ziara shambani, ufuatiliaji wa mavuno na kuwa compensated kwa kila huduma.
Sehemu za masoko: Wakulima wako hawapokei “ushauri tu” pia wanaunganishwa mara moja na wanunuzi kupitia CropSupply.com, na bidhaa zao zinafuatiliwa tangu upimaji wa udongo hadi usafirishaji.
Utapata nafasi ya kutumia vituo vyetu (Kliniki ya Kilimo) kama ofisi yako (protokali za Farmer Excellence Center), ukitumia nembo na zana zinazofahamika.
Mafunzo na miongozo: Kupitia mafunzo ya vitendo, ukaguzi na ufuatiliaji kila wiki kuhakikisha unafanya kazi kwa ubora popote bila changamoto.
Jinsi utakavyoweza kuingizia kipato:
Vipimo vya udongo → Ada ya huduma: Unatoza kwa kila sampuli na kwa kuandaa mpango wa msimu; kadri unavyohudumia mashamba zaidi, ndivyo ada zinavyoongezeka.
Huduma za kutembelea wakulima(field visits) → Malipo kwa ziara/kifurushi: Ukaguzi wa mashamba, ufuatiliaji wa magonjwa/wadudu, na “season-long checklist” hulipiwa kama ziara moja moja au kifurushi cha msimu.
Kamisheni ya pembejeo: → Ukihitaji kuwanunulia wakulima wako pembejeo zenye ubora kwa bei ya punguzo kutoka kwenye mtandao wetu wa maduka ya pembejeo, mkulima hupata punguzo na wewe unapata kamisheni halali kwa kila mauzo yanayothibitishwa.
Baada ya mavuno (CropSupply.com) → Ada/kamisheni ya uunganishaji soko: Unaposaidia kuhifadhi rekodi, ubora na ufuatiliaji hadi kuuza kupitia CropSupply.com, unapata ada ya huduma/kamisheni inapotumika.
Kukuza “portfolio” yako → Mapato yanayorudiarudia: Wakulima waliopata matokeo mazuri hukupendekeza; unaongeza idadi ya wakulima/ekari unazohudumia, hivyo kipato cha ada, kamisheni na vifurushi vya msimu kinaongezeka kila mwezi.
Kubwa zaidi ni kwamba
Huishii kuuza pembejeo bila msingi bali unatoa matokeo yanayoonekana na kuthibitishwa kwa data ya udongo, taratibu thabiti na masoko yaliyothibitishwa.
Nani anaweza kujiunga?
Mtu mwenye Diploma / BSc katika Agronomy, Crop Science, Soil Science au fani inayohusiana (au uzoefu mzuri shambani).
Mtu mwenye uwezo wa kuwahudumia wakulima na kuboresha mazao yao.
Mtu mwenye ujuzi na uwezo wa kutumia simu janja na teknolojia mbalimbali.
Mtu mwaminifu mwenye uthabiti,uwajibikaji kwa sababu utawakilisha chapa ya MazaoHub.
Maswali ya Kawaida (Q&A)
Q: Je nitanufaikaje? A: Utalipwa kwa ada za huduma (kama vipimo vya udongo, ziara shambani, mipango ya mazao), kamisheni kwa ununuzi wa pembejeo kupitia agrovets , na kamisheni kupitia huduma ya kuwaunganisha wakulima wako na masoko.
Q: Vipi kuhusu maeneo yenye mtandao hafifu je application inaweza kufanya kazi kwenye maeneo hayo pia? A: Ndio App ya Mazaohub inauwezo wa kufanya kazi bila mtandao (offline-first). Lakini mtandao unaposhika (online), unaweza kupandisha data.
Je upo tayari kuanza safari hii mpya na MazaoHub?
Jiunge leo na mtandao wetu wa kitaifa wa agrovets binafsi na maafisa ugani, na uanze safari ya kuleta mabadiliko chanya na uweze kujiingizia kipato halali.
👉 Jiunge sasa kwenye mtandao wetu kupitia link hii: https://chat.whatsapp.com/LWRyceQldTX6xpMaKt2x5A
Baada ya kujiunga, timu yetu itakutumia tarehe za mafunzo ya utangulizi, nyaraka zinazohitajika, Clinic ya MazaoHub Agricultural iliyo karibu nawe, pamoja na agrovet mshirika wako.